Mtumishi afia gesti alikoenda kujipumzisha na mrembo

NA MWANDISHI WETU

MTUMISHI wa Shirika la Umeme (TANESCO) anayefahamika kwa jina la Yahaya Abdul, mkazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni alikoenda kujipumzisha na rafiki yake wa kike.
Tukio hilo limetokea mtaa wa Ikulu, Kata ya Kawajense ambapo Mjumbe wa serikali ya mtaa huo, George Kadesi amesema, baada ya kuona umati wa watu ukiwa umezungunguka gesti hiyo na alipofika alielezwa kuwa marehemu aliingia kwenye nyumba hiyo akiwa na rafiki yake wa kike.

Kwa upande wake mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ameeleza kuwa, marehemu alifika majira ya saa 7:00 mchana na mpenzi wake lakini ameshangazwa kuona pikipiki ya mtu huyo mpaka asubuhi ikiwa pale gesti.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi , Emmanuel Tinda, amekiri kupokelewa kwa mwili wa mtu ambaye jina lake halijafahamika na uchunguzi wa kitabibu ili kubaini kifo chake unaendelea.

Aidha, mwanamke huyo ambaye alikuwa naye gesti anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news