Mwenyekiti CCM Mwanza, Waziri Dkt.Mabula watoa mkono wa pole kwa Naibu Waziri Masanja

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Anthony Mwandu Diallo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (Mb) leo wamefika nyumbani kwa Baba mdogo wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) Kata ya Nyamanoro, Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza kwa ajili ya kutoa mkono wa pole baada ya kufiwa na baba yake mdogo Mzee Charles Masanja tarehe 6 Julai, 2022.

Maziko yalifanyika Julai 9, 2022 Badugu, Wilaya Busega Mkoa Simiyu.

Post a Comment

0 Comments