Nauli mpya za meli New MV Victoria, MV Butiama kuanza kesho

NA DIRAMAKINI

AFISA Masoko Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eugenia Punjila amesema kuanzia Julai 4, 2022 bei mpya za nauli kupitia safari ya maji kati ya Mwanza na Bukoba mkoani Kagera itapanda.
Nauli mpya ambazo zinatarajiwa kuanzia wastani wa shilingi 2,445 hadi shilingi 10,000 kwa safari zitahusisha meli ya New MV Victoria (Hapa Kazi Tu) na New MV Butiama (Hapa Kazi Tu) inayoelekea Nansio i

Punjila amesema, mabadiliko hayo yanatokana na gharama gharama za uendeshaji ambazo zinawalazimisha kufanya hivyo ili kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi.

Amesema kuwa, nauli za daraja la uchumi iliyokuwa shilingi 16, 000 kwa mtu mzima imepanda hadi shilingi 21, 000 huku nauli ya watoto ikipanda kutoka shilingi 8,550 hadi shilingi 11, 000.

Pia kwa abiria wanaosafiri katika daraja la biashara ambao awali walilipa nauli ya shilingi 30, 000 sasa watalipa shilingi 40, 000 huku kwa watoto ikiwa ni shilingi 21,000.

Amesema, wazazi watakaosafiri na watoto wao katika daraja hilo sasa watawalipia nauli ya shilingi 21, 000 badala ya shilingi 15, 550 ya awali, ikiwa ni ongezeko la shilingi 5, 450 kwa safari.

Aidha, nauli za daraja la kwanza iliyokuwa shilingi 45, 000 imeongezeka hadi kufikia shilingi 55,000 huku watoto ambao awali walilipiwa shilingi 23,050 na sasa watalipiwa shilingi 26,000.

Punjila amesema, kwa upande wa New MV Butiama kwa daraja la kwanza nauli imeongezeka kutoka shilingi 10,000 kwa watu wazima hadi kufikia shilingi 12,000 huku kwa watoto ikiwa ni shilingi 7,000.

Amesema, kwa upande wa daraja la pili ambapo nauli ilikuwa ni shilingi 8,000 kwa watu wazima sasa ni shilingi 10,000 huku kwa watoto ikiwa ni shilingi 6,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news