Orodha ya waombaji waliopata ajira na vituo vyao vya kazi walivyopangiwa Wizara ya Afya leo Julai 1,2022

NA GODFREY NNKO

WIZARA ya Afya imetoa orodha ya watumishi walioitwa kazini kufuatia waombaji wa ajira za kada za afya zilizotangazwa kwenye tovuti ya wizara ajira.moh.go.tz tarehe 16 Aprili, 2022 hadi tarehe 03 Mei, 2022.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 30, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Prof. Abel N. Makubi ambapo amefafanua kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya zoezi la uchambuzi wa maombi ya kazi yaliyopokelewa kukamilika.

Prof.Makubi amesema kuwa, waombaji waliokidhi vigezo ambao majina yao yameorodheshwa kwenye orodha hii wanatakiwa kuzingatia yafuatayo;

Mosi,kuripoti katika Ukumbi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mirembe jijini Dodoma ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.

Pili kufika na cheti halisi na nakala mbili kwa kila cheti ambacho kilitumika wakati wa kuomba ajira ikiwa ni pamoja na;
i. Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
ii. Wasifu binafsi (CV)
iii. Nakala ya Kitambulisho/namba ya Uraia (NIDA);
iv. Nakala ya vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
v. Nakala ya vyeti vya taaluma pamoja na Transcript;
vi. Nakala ya Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship);
vii. Nakala ya Cheti cha usajili kutoka Baraza na Bodi husika (Valid Licence);
viii. Nakala ya Ithibati ya vyeti vya elimu na taaluma (Accreditation na
Equivalence) kutoka TCU na NECTA kwa wale waliosoma vyuo nje ya nchi
pamoja na wale waliosoma Sekondari nje ya nchi/Mitaala ya nje;
ix. Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha
kuzaliwa hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa
Msajili wa Viapo na Kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makazi;
x. Picha mbili (2) Passport Size.
Aidha, yeyote atakayeripoti na ‘Transcript’ tu au kuwa na nakala pungufu ya
vielelezo tajwa hapo juu hatapokelewa.

"Aidha, tunapenda kuwafahamisha kwamba, ajira hizi zimelenga kupunguza upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali, na kwamba uhitaji kuajiri wengine bado upo, hivyo waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili wafahamu kuwa hawakupata nafasi, hivyo wasisite kuomba tena wakati nafasi
za kazi zitakapotangazwa tena.

"Waombaji wote mnasisitizwa kuzingatia muda wa kuripoti kazini kama ilivyoainishwa hapo juu. Wizara itachukua hatua ya kujaza nafasi hizo kwa wale ambao hawataripoti kwa siku zilizotajwa hapo juu,"ameeleza Prof.Makubi, Ifuatayo ni orodha ya wanaoitwa kazini;


Orodha ya waombaji waliopata ajira na vituo vyao vya kazi walivyopangiwa BOFYA HAPA KUONA MAJINA ZAIDI NA VITUO VYA KAZI>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news