Prof.Mkenda:RUWASA ijitathmini usimamizi mradi wa maji Rombo

NA MATHIAS CANAL

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imetakiwa kujitathmini kutokana na kadhia ya kushindwa kusimamia mradi wa maji wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prf Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo Julai 26, 2022 wakati akiwa katika muendelezo wa ziara jimboni humo ambapo amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa shilingi bilioni 2.9.

Prof.Mkenda amekagua mradi huo ambao mkandarasi alisaini kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka huu 2022, lakini mpaka sasa hakuna kazi iliyokwisha kufanyika zaidi ya kuwekwa mchanga na kokoto zisizozidi hata gari moja.
Prof.Mkenda amesema kuwa, ameamua kufika na kukagua chanzo cha maji katika Mto Wona ambapo mradi huo utakapokamilika utarahisisha upatikanaji maji kwa lita milioni nne kwa siku na kupunguza kwa kiasi kikuwa tatizo la maji Rombo linaloikabili Wilaya ya Rombo.

"Tatizo namba moja, mbili, na tatu Rombo ni maji sasa mtu anayechezea mradi wa maji sielewi ana madhumuni gani na anataka wananchi wa Rombo wawe na taswira gani kwa serikali, wanamhujumu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso ambaye ni mchapakazi na kwa hili nitamualika aje aone changamoto hii,"amesema Prof.Mkenda.
Amesema kuwa, mradi huo ni sehemu ya miradi ya maji yenye jumla ya shilingi bilioni 10 iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maji Wilayani Rombo.

"Kwa kuwa sehemu hii ni ngumu kufika sio rahisi kwa viongozi kufika na kuona maendeleo ya mradi huo inakuwa rahisi kuficha mapungufu haya kwa hiyo RUWASA inabidi ijiangalie upya kwa kuwa ndio msimamizi wa mradi huu,"amesisitiza Prof. Mkenda.
Prof.Mkenda amesema kuwa, kwa sasa katika Wilaya ya Rombo, RUWASA inatia shaka usimamizi wake wa miradi ya maji hvyo amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo kutembelea Rombo ili kujionea kadhia hiyo ya ucheleweshwaji wa mradi wa maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news