Rais Dkt.Mwinyi awatembelea wajasiriamali, akabidhi bodaboda kwa vijana

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekagua shughuli za wajasiriamali pamoja na kuwakabidhi wajasriamali bodaboda katika viwanja vya Gombani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Gombani kwa ajili ya kutembelea Maonesho ya Wajasiriamali na kukabidhi Pikipiki (Bodaboda) kwa Vijana Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Pemba zilizotolewa kwa mkopo nafuu bila riba na Benki ya CRDB, akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji na Uchumi Zanzibar, Mhe. Mudrik Soranga.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo Julai 27, 2022 wakati akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kusini Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa Kikundi cha Halua Halisi Chakechake,Mohammed Saleh Ali, alipotembelea maonesho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Uwanja wa Gombani Chakechake Pemba akiwa katika ziara yake Mkoa wa Kusini Pemba.

Katika maelezo yake Rais Dkt. Mwinyi alieleza hatua tano zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha wajasiriamali wanasaidiwa ikiwa ni pamoja na kuwasaidia katika kuwapatia mtaji, soko, elimu, kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao pamoja na zana za kufanyia kazi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Waendesha Bodaboda Mkoa wa Kusini Pemba (PESIBOA), Kassim Juma Khamis, akisoma risala kwa niaba ya wajasiriamali hao, wakati wa hafla ya kukabidhiwa Pikipiki (Bodaboda) zilizotolewa mkopo nafuu na Benki ya CRDB kwa Wajasiriamali, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba. Kulia kwa Rais ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 5,000,000 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu Wasioona Wilaya ya ChakeChake Pemba (kushoto kwa Rais),Suleiman Soud Suleiman, iliyotolewa Mkopo Nafuu na Benki ya CRDB kwa Kikundi cha Mategemeo Coop Society Chakechake, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gombani, kushoto kwake ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki,Badru Iddi.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa hafla ya kutembelea Maonesho ya Bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali na kukabidhi Pikipiki (Bodaboda) kwa Jumuiya ya Waendesha Bodaboda Mkoa wa Kusini Pemba, zilizotolewa Mkopo nafuu na Benki ya CRDB, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gombani Chakechake.Wajasiriamali mbalimbali wa Mkoa wa Kusini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika hafla ya kukabidhi pikipiki (Bodaboda) kwa vijana wajasiriamali wa Jumuiya Waendesha Bodaboda Kusini Pemba (PESIBOA) iliyofanyika katika viwanja vya Gombani Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments