Rais Samia ampeleka Balozi Caroline Chipeta nchini Uholanzi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania, The Hague nchini Uholanzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus leo Julai 26,2022 uteuzi huo unaanza mara moja.

Balozi Chipeta alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 

Post a Comment

0 Comments