Rhobi Samwelly ateta na mamia ndani ya American Church in Paris (ACP)

NA FRESHA KINASA

MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT), Rhobi Samwelly amepewa fursa ya kuzungumza kueleza kazi anazofanya mbele ya kusanyiko kubwa la waumini wa The American Church in Paris (ACP).
Kanisa la Marekani huko Paris ndilo kanisa la kwanza la Marekani kuanzishwa nje ya Marekani ambalo linawakutanisha mamia ya waumini kutoka maeneo mbalimbali jijini Paris.

Miongoni mwa kazi ambazo Rhobi amekuwa akifanya kupitia shirika analoliongoza ni pamoja na mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, kutetea usawa wa kijinsia pamoja na kutetea haki za binadamu. 
Aidha, Rhobi Samwelly amewahi kutunukiwa tuzo ya Malkia wa Nguvu kutokana na juhudi zake katika mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ambapo katika Mkoa wa Mara Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) lina vituo viwili vinavyotoa hifadhi kwa wasichana ambao hukimbia aina mbalimbali za ukatili kikiwemo Kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama kilichopo Mugumu Wilaya ya Serengeti na Kituo cha Nyumba Salama kilichopo Kiabakari Wilaya ya Butiama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news