Serikali yadhamiria makubwa Sekta ya Kilimo

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha inatatua changamoto zinazokabili sekta ya kilimo ili kuwawezesha wakulima kufanya kilimo kinachoendana na teknolojia kitakachosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuchangia pato la Taifa. 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao kilichofanyika kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo, Bw. Joseph Kiraiya wakati akiongoza kikao cha majadiliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma. 

Mkurugenzi huyo amesema, Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ni mpango wa miaka 10 unaolenga kuleta mageuzi ya sekta ya kilimo (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), kuongeza uzalishaji wenye tija na kufanya kilimo kuwa cha kibiashara. Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Kilimo, Bw. Joseph Kiraiya akizungumza katika kikao cha majadiliano kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kuhusu Mkakati wa Nchi wa AGRA TANZANIA katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma.

“Mpango huu nia yake ni kuleta mageuzi kwa sekta hii kama tunavyojua ina mchango mkubwa sana katika pato la Nchi yetu hata wakulima kipato chao kitaongezeka, tutakuwa na chakula cha kutosha, usalama wa chakula na lishe,” alisema Mkurugenzi huyo. 

Aidha, Makamu wa Rais anayesimamia Sera kutoka Shirika la Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA),Dkt.Nwafor Apollos alibainisha kwa shirika hilo liko tayari kufanya kazi na serikali katika kuboresha mazingira ya kilimo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news