Siku wajenzi huru walipobadili jina la msikiti,lengo kuunganisha dini zote duniani

NA CHARLES REGESIAN

MUNGU mwenyewe ingawa hashindwi na jambo lolote, lakini hawezi kuilazimisha dhamiri ya mtu ili aitawale.

Wahenga walisema "kupanga ni kuchagua". Bahati mbaya wengi sana wamechagua kusalimisha dhamiri zao kwa viongozi wao wa kiroho na wapo tayari kukubali fundisho au agizo lolote wanalofundishwa na viongozi hao.
Lakini usalama pekee wa nafsi zetu upo katika kusalimisha dhamiri zetu kwa Mungu muumba Mbingu na Nchi ili yeye awe mtawala wetu.

Mabadiliko ya kidini na kisiasa yameendelea kuonekana katika Mashariki ya Kati baada ya mwana Mfalme Sheikh Mohammed bin Zayed Al-Nahyan ambaye pia ni mtawala wa Jiji la Abu Dhabi na Naibu Mkuu wa Majeshi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufanya mabadiliko ya jina la msikiti mkubwa jijini Abu Dhabi kutoka jina la Sheikh Mohammed bin Zayed Masjid na kuitwa jina la "Mariam, Umm Elsa" yaani " Mariam mama wa Yesu".

Lengo la kubadilisha jina la msikiti mkubwa jijini Abu Dhabi ni kuimarisha umoja kati ya wafuasi wa Imani tofauti.

Waziri wa Nchi, Sheikh Lubna Al-Quasimi alimshukuru mwana Mfalme akisema kwamba maelekezo ya kubadili jina ni maamuzi ya hekima na yanaonesha mfano mzuri katika UAE.

Mohammed Mattar Al Kaabi, ambaye ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mambo ya Kiislamu pia alimshukuru mwana Mfalme kwa uamuzi wake huo,-

Kwa upande wake,mchungaji Canon Andrew Thompson wa Kanisa la Mtakatifu Andrea kanisa hilo lililoko jirani na msikiti huo, aliiambia Shirika la Gulf News kwamba, "alifurahi baada ya kusikia habari hizo".

Akasema, "Tunashukuru kuwa tunaadhimisha jambo ambalo tupo nalo kwa pamoja katika imani zetu sote, akaendelea "Mariam, kama mama wa Yesu, ni kweli mtakatifu mfano maalum katika jamii yetu...tunatarajia kuendelea uwepo wa maelewano zaidi na majirani zetu, na tunasherehekea jina jipya la msikiti huo. Baadae kanisa la eneo la Al Ain lilifungua milango yake kwa Waislamu kwa ajili ya swala ya Magharibi.

Tukio hilo lilihudhuriwa na Waislamu wapatao 200 ambao walifanya ibada ndani ya kanisa pamoja na Wakristo.

Askofu Paul Hinder wa Kanisa Katoliki na Mkuu wa makanisa Kusini mwa Saudi Arabia ambaye ofisi yake ipo mita chache tu kutoka kwenye msikiti huo, hakubaki kimya kuonesha furaha yake kwa uamuzi huo wa mwana mfalme kubadili jina la msikiti huo, alisema , "kama Yusufu, mchumba wa Mariam, ndilo jina la Cathedral iliyopo jirani na msikiti, na sasa tunayo familia takatifu kwenye eneo hili.

Bila shaka alimaanisha kwamba kwa msikiti kuitwa jina la Mariam, Umm Elsa na jengo la Kanisa kuitwa St. Joseph Cathedral linawafanya watu wanaofanya ibada kwenye nyumba hizo kuwa ni watu wa familia takatifu, sasa tunao msikiti unaitwa Maria Mama wa Yesu na linaloitwa Yusufu.

Ni jambo jema watu kuishi pamoja na kwa umoja na amani, lakini umoja wa kweli hupatikana baada ya kufanya umoja na Mungu.

Umoja wa kweli unaanzia ndani ya moyo kabla ya kuonekana kwa nje, tunaweza kusema kuwa tuna umoja tukafanya ibada pamoja, tukabadili majina ya nyumba za ibada kwa kutumia majina ya watu mashuhuri waliopata kuwa na umoja na Mungu lakini sisi tusiwe na umoja na Mungu hivyo tukawa pamoja bila umoja.

Wajenzi huru wanasema "The great strength of our order lies in its concealment, let it never appear in any place in its own name, but always concealed by another name, and another occupation .... (Rejea ;John Robinson;Proofs of a Conspiracy 1798,Boston . 1967,page 112) wakimaanisha 'nguvu kubwa ya utaratibu wetu ipo katika kufanya kazi Kwa uficho (Siri) hebu isionekane mahali popote kwa kutumia jina lake,

"Bali ufichwe kwa jina lingine". Haijalishi ni jina zuri kiasi gani tunalitumia kwenye nyumba zetu za ibada au hata kwa kuyaita madhehebu yetu;tusipokuwa na umoja na Mungu sisi sio watu wa Mungu na umoja wetu ni umoja bandia.

Wajenzi huru hutumia kanuni kuu tatu na kwamba nguvu ya kanuni hizo ni kufanya kazi Kwa Siri, Kanuni inayowapatia mafanikio makubwa ni kanuni ya kwanza inayosema," Thesis × Antithesis =Synthesis" au "Ukweli wote" Uongo×mchache =Uongo wote, " Walibuni kanuni hii baada ya kusoma Biblia takatifu katika Yakobo 2:10 kwamba "Maana mtu awaye yote atakayeshika sheria yote (Ukweli wote) ila akajikwaa katika neno moja (Uongo mchache) amekosa juu ya yote (Uongo wote).

Mjadala wa udini wa mfumo wa kiraia au Jamhuri uliopo nchini na kwinginepo unaelekea kufikia tamati baada ya kuanza kwa harakati za kina nchi mbalimbali duniani kuondoa dhana kuwa endapo nchi haifuati sharia kamili kama inavyotajwa katika dini,nchi hiyo Iko pabaya na inahitaji kurekebishwa.

Anayejitwika jukumu la kufanya hivyo au kuingia katika harakati hiyo anakuwa shahidi,wakati maana halisi ya ushahidi ni kimshuhudia Mungu pale ambapo kuna miungu hasa ya jadi ila Kwa ukereketwa wa dini,utatu katika ukristo ukaitwa ni ibada ya sanamu,vita ikasambazwa kila mahali,kuanzia uamsho nchi za Kiarabu mwaka 2011(mwaka aliouawa Osama bin Laden).

Yako mabadiliko makubwa,wasomi wa Kiislamu wakigundua kuwa masaa machache baada ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kwamba Taifa lake linajitoa kwenye mkataba wa nyuklia ya Iran, ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe 14/5/2018, Israel ilishambulia vituo vya kijeshi vya nchini Syria.

Taarifa zilizotolewa na Israel National News tarehe 8/5/2018 zilisema kwamba milipuko ya mabomu ilionekana Kusini mwa mji Mkuu wa Damascus kwenye kituo cha kijeshi cha Iran, Rami Abdel Rahman ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Uingereza la haki za binadamu linalofanya kazi nchini Syria alisema kwamba makombora hayo yalilenga kambi za wapiganaji wa Hezbollah na jeshi la Iran na kusema kwamba, kwa uchache watu 23 ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Serikali pamoja na jeshi la Iran Revolutionary Guards, walipoteza maisha.

Kwa maneno mengine ndege za Israel zilifanya mashambulizi hayo dhidi ya jeshi la Iran wakati Rais Trump alipotangaza kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran,mkataba huo uliwekwa mwaka 2015 na umedumu kwa miaka mitatu kabla ya Trump kutangaza kujitoa, kwa upande wake kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khomeini aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Tweeter @khamenei _ir akisema' :"A few days ago Trump wrote a letter to leaders of #persian Gulf states ,which was revealed to us, He wrote:I spent $7 trilion and you must do something in return.

"The US wants to own humiliated slaves "Akimaanisha kwamba" Siku chache zilizopita Trump aliwaandikia barua viongozi wa Ghuba ya Uajemi, ambayo ilifunuliwa kwetu, Aliandika ;Nilitumia Dola trilioni 7 na ninyi lazima mfanye jambo fulani kama malipo.

"Marekani inataka kujimilikisha watumwa wa hali ya chini, barua inayodaiwa na Ayatollah kutumwa na Trump kwa viongozi wa ghuba ya Uajemi haijatambuliwa na Ikulu ya White House, ambapo msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa alisema haiwezi kuwa barua ya kiofisi. Hata hivyo, Afisa wa juu ambaye hakutaka jina lake lijulikane kutokana na kutokuwa msemaji wa Serikali, alisema kwamba uongozi wa Trump ulituma barua kwa viongozi wa ghuba ya Uajemi wiki mbili zilizopita kabla ya Trump kutangaza kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran.

Wakati kiongozi Ayatollah Ali Khamenei, akiandikia hayo ,jeshi la Iran lilirusha makombora 20 nchini Israel kutokea Syria, Hata hivyo, Israel inadai kwamba iliweza kuyazuia makombora hayo kabla hata ya kutua na kuleta madhara , Kwa mujibu wa Israel makombora mengine yalishindwa kuruka na kudondokea Syria.

Kwa miaka kadhaa sasa kiongozi wa kiroho wa Iran amekuwa akitamka "death to Israel" kumaanisha "kifo kwa Israel" na inadaiwa pia kuwa Iran imekuwa ikiunga mkono harakati za Hezbollah nchini Lebanon na Hamas kwenye mipaka ya Israel huko Gaza kwenye ukanda wa Magharibi.

Marekani inadai kuwa makundi ya Hezbollah na Hamas ni makundi ya kigaidi, kwa maana nyingine Marekani inadai kwamba Iran inashirikiana na magaidi, Tangu Iran ilipojiingiza kwenye vita vya wenyewe Kwa wenyewe nchini Syria, Israel inadai kwamba Iran imekuwa ikijaribu kuishambulia kutokea Syria.

Israel imekubali mara chache sana kuhusika na mashambulizi dhidi ya vituo vya Iran nchini Syria na imekiri kufanya mashambulizi yasiyozidi 100 tangu mwaka 2012,Israel imeapa kutoiruhusu Iran kujenga kituo cha kijeshi cha kudumu nchini Syria na ipo tayari kuingia vitani ili kuzuia jaribio hilo.


Waziri Mkuu Benyamin Netanyau alisema, "Whoever hurts us, we will hurt him sevenfold. Whoever tries to hurt us, we will act to hurt him beforehand "Akimaanisha kwamba, yeyote atakayetudhuru tutamdhuru mara saba zaidi, Yeyote anayejaribu kutudhuru tutatenda kwa lengo la kumdhuru kabla hajatenda lolote."

Kuna amri 11 za dini ya wajenzi huru zinazopingana na amri 10 za Mungu, Amri ya 11 ya dini ya wajenzi huru inasema, "If someone hurts you, ask him to stop, If he does not stop, destroy him, ikimaanisha "kama mtu akikudhuru, mwambie aache, kama akikataa, muangamize, Hapa Netanyau anatekeleza amri ya 11 ya dini ya wajenzi huru.

Hata hivyo, Netanyau alikwenda mbali zaidi ya amri ya 11 hiyo, yeye anasema hata kama mtu akijaribu kuleta madhara, wao watamdhuru kabla hajawadhuru, Lakini hivi ndivyo wafanyavyo magaidi na wanaodai kutetea ukweli kwa mtutu wa bunduki.

Yesu ambaye Wayahudi walimkataa aliagiza akisema,"Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu, lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili, Mmesikia kwamba imenenwa umpende jirani yako na umchukie adui Yako, lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi "(Mathayo 5:39, 43,44) Na katika Warumi 12:19 imeandikwa "wapenzi ,msijilipize kisasi,bali ipisheni ghadhabu ya Mungu;maana imeandikwa ,kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa,anena Bwana," Basi ni wazi kwamba yeyote anayelipiza baya Kwa baya huyo anatekeleza amri ya 11 ya wajenzi huru hata kama sio muumini wa dini hiyo.

Unaweza kuwa mkristo,muislamu ,myahudi,budha n.k ,lakini bado ukawa unatekeleza amri za dini ya wajenzi huru, wewe mbele za Mungu unahesabiwa kuwa muumini wa dini ya wajenzi huru kwa ndani, ingawa kwa nje unajiita kwa jina hilo, ukweli ni kwamba jina halimuokoi mtu.


Wakigundua kuwa amani inakuja kwa kutambua uhusiano wa kina katika vitabu, kwa mfano uwepo wa Bikira Maria kama mama aliyetukuka katika Korani na ndiyo tukio lililojiri Ufaransa.

Sikukuu ya utambulisho (au tangazo) la malaika kwa Mama Maria kuwa atazaa mwana na kumwita Yesu, kwa maana ndiye atakayewaokoa watu na dhambi zao. Waislamu katika nchi nyingi duniani wanachukua vipande vya habari tofauti kuhusiana na Yesu.

Siku hizi ni kawaida kuwaona sheikh na mchungaji wanashirikiana kuelezea maandiko yanavyosema, kuwa Masihi ndiye atakayekuja kuuokoa ulimwengu, Kuna toleo la 20 la gazeti la Risala ambalo mwandishi anatoa maelezo ya fikra ya mwanazuoni mahiri wa Algeria ambaye anaelezea jinsi itikadi ya U-Wahabbi (iliyoanza na Sheikh Mohammed ibn Abdulwahhab wakati wa kuanzishwa kwa ufalme wa Saudia miaka ya 1920 ilipoanguka himaya ya Kiislamu ya Ottoman, ya waturuki) ilivyoharibu fikra za waislamu kote duniani.

Suala ni kuwa tofauti na mzungumzaji katika meseji hizi, anadhani kuwa makundi ya kijihadi kote duniani yalianzishwa na Marekani na CIA kwa malengo yao ili kuupakazia uislamu. Na suala tata la kuanguka kwa majengo pacha ya WTC jijini New York Septemba 11, 2001liliweka pilipili nadharia hiyo, ikaenea kote kuwa hakuna ugaidi, ni njama tu.

Ila mabadiliko makubwa yameanza kote duniani kutokana na mshtuko ambao waislamu waliupata kutokana na vitendo vya kinyama vya kundi linalojiita Dola ya Kiislamu, lililokuwa likiacha milima ya maiti popote lilikopita, likikuta m-shia, m-kristo, m-rasta, m-kurdi, m-Hindu, m-Budha, m-Bahai, mradi siyo Muislamu, Sunni wa dhehebu la Wahabbi anakatwa kichwa.

Ukaanza mjadala wa aina fulani si wa kina sana katika jarida la Saphirnews la kifaransa linalowekwa katika mtandao kuwa, labda kuna dhambi ya asili ambayo uislamu haujaitambua na ndiyo maana wanazuoni Ulaya wakaanza kurudi katika Korani, kuangalia mwokozi wa dunia ni nani hasa, kama ni sharia kama ilivyo au ni Masihi, na ndicho ambacho kinaenezwa sasa, hasa kwasababu Mahdi anapokuja anakuja na Yesu, siyo peke yake,akivaa joho la Sheria kama Dola ya Kiislamu itakavyo.

Hivyo kufanyika ibada ya pamoja kati ya waislamu na wakristo katika Kanisa Katoliki mjini Venissieux mnamo Aprili 8 mwaka 2018 Kwa kumbukumbu ya "Sikukuu ya Announciation" yaani announcement, tangazo alilopewa Bikira Maria la kuzaliwa Yesu.

Walikutana katika Kanisa la Epiphania, wakipokewa na Paroko, Regis Charre na Rais wa msikiti wa Al Forgane,Imam Mourad Merabet na wafuasi wao katika Jimbo hilo kandokando ya jiji la Lyon katikati ya Ufaransa.

Walifanya sala ya pamoja, wakitoa masomo kutoka katika biblia na Korani,yote yakilenga sifa za Mama Maria mbele za Mungu ,na baadae kuwa na karamu ya pamoja katika eneo hilo. Kwa suala hili la jinsi Yesu alivyozaliwa hakuna tofauti ya fikra kati ya waislamu na wakristo ,kuwa alizaliwa Kwa muujiza alioufanya Mungu,na tofauti zinakuja katika undani wa kitheolojia wa mafundisho yake na ngazi yake katika mbingu.

Hilo halikuwa katika mazungumzo ila undani wa kutambua suala hilo na kwa maana hiyo, Wakristo kuondoa hisia kuwa Korani imeandikwa na mwanadamu tu aitwaye Muhammad, wakati sivyo,ni udhaifu tu kuelewa kwanini Mungu ameshusha vitabu au mtiririko zaidi ya mmoja wa Vitabu vya dini.

La msingi ni kuwa mitiririko hiyo ni sehemu ya imani na mazingira yake kihistoria,na la ziada ni kuwa dini yoyote Ile isitake kutawala ,au kutumia dola kwa manufaa halisi ya dini au watu kujinufaisha kwa mgongo wa dini.

Mfano ni kupinga Jamhuri kama mfumo wa kanisa,au kutaka katiba mpya ambako makanisa yatatumia misamaha ya kodi bila kuulizwa na kama Kuna swali liamuliwe na Bunge, na siyo liwe katika mamlaka ya Rais na Kwa maana hiyo mawaziri wake kuhoji,kuchukua hatua inayoliudhi kanisa.

Mtandao wa Saphirnews ulisema kuhusiana na tukio hilo kuwa Paroko Regis Charre alieleza uhakika wake kuwa ibada hiyo ya pamoja itaendeleza kwa kiasi kikubwa majadiliano kati ya waislamu na wakristo katika mji huo, na kwingineko ambako habari hizo zitafika.

Pia watu wa kujitolea,wakiwa na furaha kubwa ya kufanyika kwa ibada hiyo na maelewano hayo, wamependekeza kuundwa vikundi vingine vya makutano (katika nyanja tofauti za imani, kumbukumbu) Wanaparokia ya Epiphania tayari walialikwa mwezi wa Juni 2018 kushiriki katika futari ya kumaliza mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Kuunganisha dini ni tukio la kumi kati ya matukio yaliyopangwa na wajenzi huru, hapa nia ni kupata dini moja duniani kote ya kipagani, katika kufanikisha hili viongozi wakuu wa WCC, walikutana huko Malaysia kwa muda wa siku tatu kufikia muafaka wa kutoa waraka unaohusu kuunganisha makanisa yote duniani,(Rejea Msemakweli toleo Na.777 julai 15, 2012).

Naye Imaad Ali wa msikiti wa Al-Salaam nchini Canada aliwaalika wakristo katika ibada ya ufunguzi wa mwezi wa Ramadhani na kutoa wito duniani kote kwa kuwataka wakristo kuungana na waislamu katika mfungo wa Ramadhani,ndani ya msikiti wa Al-salaam. Immad Ali ambaye alisomea kozi inayoitwa "Trinity" katika Chuo Kikuu Cha Western University huko Langley aliwataka waumini wa kikristo waungane na wenzao waislamu katika ibada za kila siku.

Katika Chuo Kikuu Cha Simon Frazer University akihutubia katika hotuba zilizofanyika kabla ya mwezi wa Ramadhani,Bruce Lawrence ambaye ni mkristo wa dhehebu la Anglican aliyesomea masomo ya dini ya uislamu katika Chuo Kikuu Cha Aga Khan,alisema "I am an Anglo-Mohammedan,a Christian who believes in the Koran akimaanisha kwamba yeye ni m-kristo anayeamini Korani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news