Simbu aipa heshima Tanzania mbio ndefu Jumuiya ya Madola

NA DIRAMAKINI

MWANARIADHA wa Mbio Ndefu Marathon (42KM),Bw. Alphonce Felix Simbu amenyakua Medali ya Fedha kwa kukimbia muda (2:12:29) nyuma ya raia wa Uganda, Victor Kiplagat (2:10:55) na Mkenya wa Tatu kwa muda (2:13:16).
Ni kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika jijini Birmingham, Uingereza leo Julai 30,2022.

Kwa upande wa wanawake, Failuna Matanga amemaliza wa sita kwa muda (2:33:29) kwa Marathon, huku Hamisi Athumani Misai akishika nafasi ya nane kwa wanaume Marathon muda (2:15:59) huku Jackline Sakilu akimaliza kwa shida baada ya kuumia mguu.

Post a Comment

0 Comments