Simbu,Taifa Stars watoa tabasamu kwa Watanzania leo

NA DIRAMAKINI

MAPEMA mwanariadha wa Mbio Ndefu Marathon (42KM),Bw.Alphonce Felix Simbu alianza kwa kuwapa tabasamu Watanzania baada ya kunyakua Medali ya Fedha kwa kukimbia muda (2:12:29) nyuma ya raia wa Uganda, Victor Kiplagat (2:10:55) na Mkenya wa Tatu kwa muda (2:13:16).

Ni kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika jijini Birmingham, Uingereza leo Julai 30,2022.
Wakati nderemo zikiwa hazijapoa, Taifa Stars imeiwezesha Tanzania kusonga mbele katika kuwania tiketi ya Fainali za CHAN mwakani baada ya ushindi wa 2-1 leo dhidi ya Somalia.

Ni kupitia mtanange wa nguvu uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Julai 30,2022.

Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Abdul Sopu dakika ya 34 na Dickson Job kwa penalti dakika ya 64 huku la Somalia likifungwa na Farhan Ahmed dakika ya 47.

Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza katika dimba hilo.

Post a Comment

0 Comments