Uchaguzi Mkuu Yanga SC warudishwa nyuma siku moja

NA DIRAMAKINI

KAMATI ya Uchaguzi ya Yanga imeirudisha nyuma kwa siku moja Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kutoka Julai 10 hadi 9, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Wakili Malangwe Mchungahela amesema sababu za kurudisha nyuma uchaguzi huo ni kupisha sikukuu ya Eid El Haj ambayo inatarajiwa kufanyika Julai 10, 2022.

"Uchaguzi Mkuu utafanyika tarehe tisa mwezi huu wa saba,2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere," amesema Wakili Ally Mchungahela Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Yanga SC.
 
Amesema, wagombea wanatakiwa kufanya kampeni kwa muda wa siku tano, "na leo baada ya mkutano huu na Wanahabari nitakuwa nimezindua rasmi kampeni kuanza leo,"amesema.
 

Post a Comment

0 Comments