Mwanamke usithubutu, akitaka mwambie NO! NO! NO!

NA DIRAMAKINI

KILA mmoja wetu anatambua wazi kuwa, ndoa ni muhimu, na huwa muhimu kwa sababu ni kitu kinachowaunganisha mume na mke na kuanzisha familia, na huleta baraka nyingi kama vile watoto na nyinginezo nyingi.
Tendo la ndoa ni moja wapo ya kiunganishi kikubwa ambacho huwa kinafanikisha wanandoa kuanzisha familia. Na ni msisitizo pia uliowekwa katika vitabu vitakatifu mfano Biblia, rejea 1 Wakorintho 7:3-5, "Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake, Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe. Vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

Jambo ambalo ni la msingi, ambalo ni muhimu kwetu sote kulifahamu, ni kwamba tendo la ndoa au kujamiana siyo dhambi ikiwa linafanywa ndani ya ndoa. 

Mungu ndiye aliyempa mwanadamu zawadi hii ya tendo la ndoa. Wapo watu wengi ambao wanalichukulia tendo la ndoa kuwa ni kitu kiovu na wamelazimika kutenda kinyume na maelekezo ya Mungu.

Hata hivyo ni muhimu kwetu kuelewa kwamba tendo la ndoa ni tendo takatifu kwa wana ndoa na hupaswi kujisikia mchafu unapokutana na mkeo au mumeo, ila tu pale ambapo mmoja wenu analazimisha kufanya kinyume na maumbile, yafaa kukataa kwa kuwa hayo si maelekezo ya Mungu bali matamanio na matakwa ya wanadamu.

Ukijifanza mjuzi na kuamua kufanyiwa kinyume na maumbile, tarajia kukumbana na mateso sita ambayo utayajutia maishani mwako daima;

NO! NO! NO!

Mosi,mwanamke anayefanyiwa mchezo huu hupata matatizo makubwa wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa mfululizo wakati akijaribu kumsukuma mtoto. 

Tukio hili humsababishia aibu kubwa mwanamke, kiasi cha kumshushia hadhi yake mbele ya 
jamii. 

Pili,anaweza kumuua mtoto kwa vile kila akimsukuma atoke, pumzi hukata kutokana na misuli inayofahamika kwa jina la ‘sphincter’ kulegea na kusababisha ambane mtoto. 

Tatu, umri unaposonga, haja kubwa hutoka bila kizuizi kutokana na misuli ya sphincter inayobana njia ya haja kubwa kulegea. 

Nne,inaweza kusababisha saratani ya eneo hilo ‘cancer of colon’. 

Tano,ugonjwa wa UTI, yaani uambukizi kwa njia ya mkojo, huwa sugu, maana akitokea mwanaume alifanya kitendo hicho kisha akafanya ngono kama kawaida, bakteria wanaoishi sehemu hiyo wanaingia na kuwa na madhara makubwa. 

Jambo la Sita, hasara yake kubwa, mwanaume anayekufanyia mchezo huwa hawezi kukuoa, pia ni rahisi kukutangaza kwa jamaa zake na kuonekana kituko mbele za watu, kama umeolewa heshima yako hupungua ndani ya ndoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news