Ufanisi wa jeshi wakonga moyo wa Rais Dkt.Mwinyi, kupewa kazi ya kujenga masoko

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inayajenga masoko ya Jumbi, Mwanakwerekwe na Chuini kupitia Jeshi a Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Salum Masoud Attai alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Soko la Samaki Malindi linalojengwa na kampuni kutoka Japan,wakati akiendelea na ziara yake ya Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo. (Picha na Ikulu).

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti katika mwendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ambayo leo imefikia tamati.

Katika maelezo yake Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kwamba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua uamuzi huo baada ya wawekezaji binafsi kushindwa kujenga masoko hayo.

Amesisitiza kuwa, ujenzi huo utafanyika hivi karibuni na kukitaka kikosi cha JKU, kisije kumuangusha kwani azma yake hivi sasa ni kukipa miradi kadhaa ya ujenzi kikosi hicho baada ya kuonesha umahiri mkubwa na nidhamu katika utendaji wao wa kazi.

Rais Dkt. Mwinyi alikipongeza kikosi cha JKU na kueleza jinsi alivyoridhika na utendaji kazi wa kikosi hicho kwa wakati huku akiahidi kukipa kazi ya ujenzi wa skuli ya sekondari ya Mtopepo ambayo mkandarasi wake alimsimamisha juzi huku akitaka pale ajira zitakapoanza vijana wote waliojitolea kupitia kikosi hicho waajiriwe mwanzo.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Mkoa huko Lumumba yenye ghorofa sita, alieleza azma ya Serikali ya kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo sambamba na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Rais Dkt.Mwinyi alieleza kwamba hivi sasa Serikali anayoiongoza inakwenda katika hatua mpya kwenye sekta ya afya huku akiahidi mazingira na maslahi mazuri ya wafanyakazi wa sekta hiyo pamoja na wengine wa sekta ya umma.

Aliahidi kuwepo kwa hospitali za Mikoa katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba ambazo zitakuwa zikitoa huduma za kisasa.

Nao uongozi wa Wizara ya Afya ulimpongeza Rais Dkt. Miwnyi kwa juhudi zake hizo na kuwaomba wananchi waendelee kumuunga mkono kwani amekusudia kuiletea maendeleo endelevu Zanzibar.

Akiwa katika eneo la Wajasiriamali mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya Wajasiriamali wa kusarifu mbao alisema kuwa Serikali imeamua kwa makusudi kuwawekea mazingira mazuri wajasiriamali ili waweze kufanya shughuli zao vizuri ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Alisema kwamba wakati umefika Zanzibar iwe na maeneo maalum kwa ajili ya biadhaa maalum ikiwa kwa lengo la kuuweka mji katika hali ya usafi pamoja na kuwarahisishia wananchi kujua mahala maalum pakwenda kununua bidhaa wanazozitaka.

Alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga fedha maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya michezo na kuliahidi Jimbo la Kwamtipura nalo kufaidika na fedha hizo. Pia, Rais Dkt. Mwinyi alikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayoendelea na ujenzi huko Chumbuni.

Mapema mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa skuli ya msingi ya ghorofa mbili huko katika eneo la Bint Hamrani alieleza azma ya Serikali ya kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa skuli za kisasa ili kupunguza idadi ya watoto madarasini.

Wakati huo huo, Rais Dkt.Mwinyi alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki liliopo Malindi na baadae aligawa boti za uvuvi pamoja na boti kwa ajili ya wakulima wa mwani pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya madau.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba ndoto za uchumi wa buluu zinaanza kutekelezeka na kuyataja mambo makubwa matano yanayoimarisha sekta hiyo yakiwemo zana, soko, uhifadhi wa samaki, bandari maalum za uvuvi pamoja na viwanda.

Rais Dkt. Mwinyi alieleza azma ya Serikali ya kutoa boti 577 kwa ajili wa wavuvi wa Zanzibar pamoja na hatua za kujenga masoko zaidi huku akieleza hatua za ujenzi wa kiwanda cha mwani huko Pemba na baadae kujengwa hapa Unguja.

Alisema kuwa Serikali imewakabidhi benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwa kutambua kwamba wana uzoefu mkubwa huku akieleza jinsi Serikali ilivyobeba riba katika mikopo ya fedha kwa wajasiriamali.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi aliweka jiwe la msingi katika eneo la maduka la Darajani Bazaar na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika wka ujenzi huo watakaowekwa kufanya biashara ni wale waliokuwepo awali na baada ya hapo ndio watapewa wafanyabiashara wengine.

Alieleza kwamba Serikali tayari imeshawawekea mazingira mazuri wajasiriamali wakiwemo wafanyabiashara huku akitumia fursa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news