Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Julai 20,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2753.62 na kuuzwa kwa shilingi 2782.31 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 9.83 na kuuzwa kwa shilingi 10.43.
Hayo ni kwa mujibu wa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Julai 20, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 

Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.23 huku shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.58 na kuuzwa kwa shilingi 0.61.

Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2347.30 na kuuzwa kwa shilingi 2371.70 huku Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2292.96 na kuuzwa kwa shilingi 2315.89.

Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) ikinunuliwa kwa shilingi 624.29 na kuuzwa kwa shilingi 630.48.

Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 134.24 na kuuzwa kwa shilingi 135.24 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.36 na kuuzwa kwa shilingi 19.52. 

Aidha, Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 340.07 na kuuzwa kwa shilingi 342.36 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 16.67 na kuuzwa kwa shilingi 16.83.

Post a Comment

0 Comments