Wakiri Tanzania imepiga hatua kubwa uongezaji thamani madini Afrika

NA MWANDISHI WETU

WATAALAMU kutoka nchi zinazozalisha Madini ya Almasi Afrika (ADPA) wamefurahishwa na mfumo wa mafunzo yanatolewa na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).
Wataalamu hao, wamekitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha baada ya kufika jijini humo kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa Tatu wa ADPA unaoanza leo Julai 28,2022.

Naye, Maurice Miema kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema, Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo la uongezaji thamani madini ambapo imeweza kuanzisha kituo cha mafunzo ya kuongeza thamani madini na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Aidha, Miema amesema Tanzania ni nchi inayofaa kuigwa na nchi zingine za Afrika baada ya kuona uwekezaji mkubwa katika vifaa na mashine za ung'arishaji, ukataji na utambuzi wa madini ya vito.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Daniel Kidesheni amesema timu ya wataalamu hao umefika kituoni hapo kwa lengo la kujifunza na kushuhudia shughuli za uongezaji thamani madini zinavyofanyika.

Kituo cha TGC ambacho kwa Afrika kipo Tanzania pekee kinatoa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo ukataji na ung'arishaji wa madini ya vito, utambuzi wa madini ya vito na usonara ambapo kwa sasa kuna zaidi ya wanafunzi 100 wanaosoma ngazi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news