Waziri Dkt.Mabula ashiriki mkutano Mkuu wa 41 wa Shelter Afrique nchini Zimbabwe

NA MUNIR SHEMWETA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt. Angeline Mabula anahudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 41 wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa Victoria Falls Magharibi mwa Zimbabwe.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akishiriki Mkutano Mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe jana.

Tanzania ni mwanachama wa Taasisi ya Shelter Afrique na inahudhuria mkutano huo kwa kuwa ina haki ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya taasisi hiyo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akichangia mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea kwenye mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe jana.

Shelter Afrique ni Taasisi ya fedha inayoundwa na serikali za nchi za Afrika kwa kushirikiana na Benki ya Afrika ambazo zinachangia mtaji kwa kununua hisa na kujenga mtaji unaotumia na nchi wanachama katika shughuli za maendeleo ya nyumba na miji kwenye Bara la Afrika.

Kauli mbiu ya mkutano huo unaotarajiwa kumalizika tarehe 29 Julai 2022 ni Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira jumuishi ya Ujenzi ( Climate Change and the Built Environment) ambapo Tanzania kwenye mkutano huo inawakilishwa na Waziri wa Ardhi, Dkt.Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Uendelezaji Milki, Lucy Kabyemela. Makamu wa Rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwaziri kutoka nchi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula (wa tano kushoto mstari wa mbele) pamoja na viongozi waandamizi wa Taasisi ya Shelter Afrique wakati wa Mkutano Mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi hiyo unaoendelea katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe jana.

Mkutano mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique ni moja ya shughuli muhimu za taasisi hiyo katika mikakati yake ya kipindi cha mwaka 2020- 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news