Waziri Balozi Dkt.Chana afanya uteuzi Mwenyekiti, wajumbe wa Bodi ya Wakala Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb), amemteua Bw. Imani Joel Kajula kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT) kwa kipindi cha miaka mitatu. 
Mhe. Balozi Dkt.Pindi H. Chana amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5 (4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245 kikisomwa kwa pamoja na Aya ya 2.2 ya Amri ya kuanzishwa kwa Chuo hicho cha Taifa cha Utalii. Aidha, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT): -

1:Prof. Wineaster Anderson, Prof. Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Shule ya Biashara; 


2:Bw. Matendo Bwire Manono, Wakili Mkuu II, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; 


3:CPA. Suzana Steve Chaula, Mhasibu Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE); 


4:Bw. Enock Robert Wagala, Mkurugenzi wa Mipango, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA);

5:Bibi Gerwalda Florence Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). 

Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Julai, 2022 hadi 11 Julai, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news