Waziri Balozi Dkt.Chana atembelea Serengeti

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt. Pindi Chana ametembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na kupata maelezo juu ya kituo cha kutoa habari kidijitali (Serengeti Media Center) kinavyofanya kazi ya kutangaza vivutio, shughuli za hifadhi na za jamii zinazozunguka hifadhi hiyo.
Dkt. Chana amepongeza TANAPA kwa kazi nzuri inayofanya na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya hifadhi na shirika kwa ujumla.

Awali, Dkt. Chana alikutana na Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ambapo Mkuu wa Hifadhi hiyo Kamishna wa Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai alitoa taarifa fupi kuhusu hifadhi.
Naye, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA, William Mwakilema alimshukuru Waziri Chana kwa kutenga muda na hasa kutembelea maeneo haya ili kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii zinavyofanyika.Kituo cha Serengeti Media Centre (SMC) kimeshaanza kufanya kazi na watalii wameanza kukitumia kupata taarifa mbalimbali za hifadhi na kinatarajiwa kufunguliwa rasmi hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments