Waziri Mkuu Boris ang'atuka

LONDON-Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametangaza kujiuzulu kama kiongozi wa Chama cha Conservative na kuruhusu mchakato wa kutafutwa mrithi wake kama Waziri Mkuu kuanza mara moja.
Boris Johnson. (Picha na AP).

Uamuzi huo ameufukia leo Julai 7, 2022 baada ya kujikuta katika wakati mgumu huku wabunge kadhaa wa chama chake wakimtaka aachie ngazi mara moja.

Pia zaidi ya Mawaziri 50 wamejiuzulu serikalini katika kipindi cha siku mbili zilizopita baada ya kuandamwa na kashfa mbalimbali.

"Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani,Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani.Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.

“Mchakato wa kumchagua kiongozi huyo mpya uanze sasa na leo nimeteua baraza la mawaziri kuhudumu kama nitakavyofanya hadi kiongozi mpya atakapokuwapo,”amesema Boris Johnson.

Baada ya siku za kupigania kazi yake, Johnson aliyekumbwa na kashfa alikuwa ameachwa na washirika wote isipokuwa wachache baada ya kashfa za hivi karibun i kuvunja nia yao ya kumuunga mkono.
"Kujiuzulu kwake hakuepukiki," Justin Tomlinson, naibu mwenyekiti wa Chama cha Conservative, alisema kwenye Twitter. "Kama chama lazima tuungane haraka na kuzingatia yale muhimu. Hizi ni nyakati ngumu katika nyanja nyingi."

Chama cha Conservative sasa kitalazimika kumchagua kiongozi mpya, mchakato ambao unaweza kuchukua wiki au miezi kadhaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news