Waziri Simbachawene awahamasisha wananchi kushiriki Sensa ifikapo Agosti 23

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa wananchi kujiandaa kwa zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuwa na kumbukumbu ya taarifa za watu waliolala katika makazi yako usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi 8 Mwaka 2022. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa kata ya Mbuga katika jimbo lake la uchaguzi. 

Sensa ya watu na makazi inasaidia serikali kupata idadi ya watu na kupanga mipango ya miradi ya maendeleo kulingana na uhitaji. 

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza katika Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha mbuga jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. 

“Hata kama watu watatoka ni vizuri akabaki mtu mwenye kumbukumbuku za watu waliolala katika nyumba yake ili kupata takwimu sahihi alisema Waziri” .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akimpongeza mwanafunzi wa darasa la awali Gidion Pwereza wa shule ya Igulwi baada ya kuonesha umahiri wake katika kutamka methali za Kiswahili alizokuwa anaulizwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akifurahia ngoma ya utamaduni ya Mangala katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mbuga kata ya Mbuga. 

"Naomba muendele kuwafahamisha wale ambao hawafahamu ili nao wawe na ufahamu na tuendelee kukumbushana kadri tunavyoelekea kwenye zoezi hili la sensa. 

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi Million mia kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, barabara, 

“Nitoe rai kwa watendaji kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ili ujenzi wa miundo mbinu uendane na thamani ya fedha iliyotolewa. Kuwe na Mtu maalumu anayesimamia ili aweze kuutolea taarifa sahihi inapohitajika alisema Waziri” 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari ya Mbuga baada ya kukagua ujenzi wa miundo mbinu ya maabara ya fizikia na bailojia katika shule hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akimjulia hali Mgonjwa katika Kituo cha afya cha Saint Gema kilichopo Kijiji cha Lumuma. 

Awali katika salamu za shukrani Mwalimu Justine Maganga Mkuu wa shule ya sekondari Mbuga ameshukuru Waziri kwa miradi ya ujenzi wa madarasa matatu na madawati 150 pamoja na viti vyake, ukarabati wa jengo la maabara fizikia maabara ya fizikia na kemia pamoja vifaa vyake, jambo ambalo limewezesha wanafunzi kufanya mafunzo ya vitendo katika masomo hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news