Afisa Mipango mbaroni kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 15

NA DIRAMAKINI

AFISA Mipango Miji wa Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi, Dickson Mwenda (37) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa Kibaoni wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema mtuhumiwa anadaiwa kumbaka mtoto huyo ndani ya gari lake lenye namba za usajili T 927 DMC.

Amesema kuwa, tukio hilo la unyanyasaji wa kingono lilifanyika Agosti 13, 2022 majira ya saa moja na nusu jioni huko katika Kijiji cha Kibaoni Kata ya Kibaoni wilayani humo.

Pia ameongeza kuwa, mama wa mtoto huyo alikuwa baa akipata vinywaji na mtuhumiwa ambapo baada ya muda alimuomba awapeleke watoto wake nyumbani ambao walikuwa wawili kwa maana ya mtoto aliyebakwa na mdogo wake.

Kamanda Makame ameeleza kuwa, mtuhumiwa alipofika njiani alisimamisha gari na kumbaka mtoto huyo.

Ameongeza kuwa, baada ya tukio hilo taarifa zilipelekwa katika kituo cha Polisi na baadae mtuhumiwa alikamatwa huku akibainisha kuwa, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakama kujibu tuhuma zinazomkabili muda wowote.

Post a Comment

0 Comments