Balozi Prof.Kilagi awataka Watanzania kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana Brazil

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Prof. Adelarous Kilangi amewataka Watanzania kuzitumia fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini Brazil hususani kwenye Sekta za Kilimo, Biashara, Uwekezaji na Mifugo ili kujiendeleza kiuchumi.
Mheshimiwa Balozi Kilangi ametoa kauli wito huo leo Agosti 31, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari nchini kwa njia ya Mtandao wa Zoom, kutokea nchini Brazil ambapo alitumia fursa hiyo kueleza matunda ambayo Tanzania inaweza kuyapata kupitia ushirikiano wake na Brazil.

"Miongoni mwa fursa zilizopo Brazil ni kwenye Sekta ya Kilimo hasa kilimo cha maharage ya soya, mtama na mahindi ya njano, kuna kampuni tumewasiliana nayo kutoka China imekuja Tanzania, imeanza kulima soya na tunatarajia itaanza kulima maharage ya njano na mtama, kwa hiyo wakulima wetu Tanzania wanaweza kuanza kulima mazao haya,"amesema Balozi Prof. Kilangi
Kuhusiana na suala kukabiliana na upandaji wa gharama za mafuta na nishati, Mhe.Balozi Kilangi amewashauri wadau wa kujikita zaidi kwenye uzalishaji wa gesi aina Ethanol ambayo imesaidia kupunguza gharama ya bei ya mafuta Brazil.

"Kwenye mafuta na gesi Ubalozi tulitembelea kiwanda kikubwa cha kuzalisha ETHANOL hapa Brazil, watawekeza Tanzania, tunashauri wadau waitumie fursa hii ya kuzalisha Ethanol, kwa sababu wakati Dunia nzima mafuta yakiwa yamepanda Brazil, Petroli inauzwa kwa bei ya chini na sababu kubwa ni wenzetu waliongeza uzalishaji kwenye Ethanol,"ameongeza Balozi Prof. Kilangi.

Post a Comment

0 Comments