FIFA yaahidi neema kwa Tanzania

NA JOHN MAPEPELE

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amesema FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania.

Akiongozana na wachezaji mahiri wa zamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na
mwamuzi Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania.

“Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga, lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine,”amefafanua Mhe. Mchengerwa.

Aidha,Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo.

Mhe. Mchengerwa amepokea viongozi mbalimbali wa juu kwenye mashirikisho ya Soka duniani na kufanya vikao vya kuendeleza michezo ambao leo wanahudhuria mkutano Mkuu wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha.

Aidha,Mhe. Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuendelea kuimarisha mahusiano na mashirikiano na nchi mbalimbali ambazo tayari ziliahidi kuendeleza mashirikiano katika sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni.

Mkutano huu wa kihistoria unatarajiwa kuhudhuria na zaidi ya watu mia tano na waandishi wa habari zaidi ya mia moja huku ikitarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu bilioni moja.

Tayari viongozi wakuu wa mashirikisho yote ya Soka kutoka mabara yote wamewasili na Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news