IJP Wambura afanya mabadiliko ya makamanda wa polisi leo Agosti 12, 2022

NA GODFREY NNKO

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa nchini.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 12, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, IJP Wambura katika mabadiliko hayo amemuhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Pili Omary Mande ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Ruvuma kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi.

ACP Mande anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Marco Godfrey Chillya ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Joseph Konyo ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, IJP Wambura amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Gaudiunus Felician Kamugisha kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Abdallah Haji Seti aliyehamishiwa makao makuu ya Polisi Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news