Kamati yakaribisha maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa mwaka 2022.

NA GODFREY NNKO

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imewaalika wadau kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa mwaka 2022.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 18, 2022 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

"Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (public hearing) utafanyika siku ya Jumatano tarehe 31 Agosti, 2022 saa 5:00 asubuhi katika Ukumbi Na.9 uliopo jengo la utawala Ofisi ya Bunge, Dodoma,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Muswada huo, kufika na kuwasilisha maoni yao kabla ya Muswada huo haujapelekwa katika hatua nyingine.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa, kamati itapokea maoni kwa njia ya Posta au kwa barua pepe kwa anuani za;

Katibu Mkuu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
Mtaa wa Makole,
S.L.P. 941,
41105 DODOMA.

Barua pepe:cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz

Wakati huo huo taarifa hiyo imefafanua kuwa, muswada huo unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz

Post a Comment

0 Comments