Kocha Nabi aongezewa kandarasi Yanga SC

Kocha Mtunisia, Nasredine Mohamed Nabi akiwa na Rais wa Yanga baada ya kusaini mkataba wa kuendelea kufundisha mabingwa hao wa Tanzania kufuatia msimu mzuri uliopita akiiwezesha kushinda mataji yote nchini.
Mwaka jana baada ya kuingia kandarasi ya kwanza, mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa utambulisho, Nabi aliweka wazi kwamba anaitambua Yanga kwa kuwa alikuwa anaifuatilia muda mrefu jambo ambalo halimpi tabu.

“Mimi ni kocha wa vitendo, sipendi porojo wala bla bla bla hapana kwangu ni kazi nataka Yanga iwe timu kubwa. Ninaijua vizuri na nina amini kwamba nitafanya vizuri hivyo ninashukuru kwa nafasi ambayo nimeipata nitatoa ushirikiano na kufanya kazi kwa ufanisi,”alisema.

Aidha, kocha huyo ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa miongoni mwa timu ambazo alifundisha ni pamoja na Al Merrikh ya Sudan ambayo iliishia hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika na msimu ulioisha aliiwezesha klabu hiyo kufanya vema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news