Max Bushoke, Fresh Jumbe, Benno Villa, Abdalah Gama wairudisha Sikinde Original

NA DIRAMAKINI

KUNDI la Muziki wa dansi la Orchestra Sikinde Original, Jumatatu hii linaachia wimbo wake wa pili mpya uitwao MCHEPUKO maarufu kama "NYUMBANI KUMENOGA".
Sikinde Original inaundwa na wanamuziki mbalimbali waliowahi kupigia bendi ya DDC Mlimani Park na ambao wengine Bado wanafanya kazi na bendi ya Mlimani Park na bendi zinginezo.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Fatuma Munene amesema wimbo huo unazungumzia Kisa cha wanandoa ambao hawakuwa sawa na kuangukia kwa mchepuko ambapo Bado mambo hayakuwa sawa hadi pale mwenza anapomwambia mwenzie arudi nyumbani Kumenoga.

Munene alisema Sikinde Original ina lengo la kurejesha ladha ile ya Sikinde ya miaka ya nyuma ikachanganya na vionjo vya kisasa.

"Kuna wanamuziki wengi waliopita Sikinde watatumika katika kutengeneza albamu ya kundi hili na katika albamu wimbo wa kwanza ni Mchepuko....huko mbele zipo suprise nyingi sana, tujachojaribu kufanya ni kuinua muziki wa dansi ambao wapo wanaosema umeshuka,"
Katika wimbo waimbaji ni wakongwe Bennovilla Anthony, Maximilian Bushoke, Abdalah Hemba, Athuman Kambi na Fresh Jumbe Mkuu.

Kwa upande wa ala magitaa yamepigwa manne ambapo Solo limepigwa na Omary Seseme, Second Solo, Mkongwe Abdalah Gama, rythim Mjusi Shemboza wakati Bass ni Bonny Chande.

Juma Choka ameshiriki kwenye Drums huku Ibrahim Chande kwenye Trumpet. Huu ni wimbo wa pili kutolewa na Orchestra Sikinde Original. Wimbo wa kwanza ni Sensa ambao ni maalum kuhamasisha zoezi la kuhesabiwa. Video ya Mchepuko iko mbioni kuachiwa pia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news