🔴LIVE: YANGA SC vs SIMBA SC NI DERBY YA KARIAKOO

KIKOSI cha kwanza cha Simba kitakachoanza dhidi ya Yanga mchezo wa Ngao ya Jamii leo Agosti 13 langoni kipa namba moja Aishi Manula amekosekana hivyo majukumu yapo kwa Beno.
Maki Zoran Kocha Mkuu wa Simba ameanza namna hii ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ushindani ndani ya kikosi cha Simba:-Beno Kakolanya, Israel Mwenda, Mohamed Hussein,Henock Inonga, Mohamed Quattra, Jonas Mkude, Pape Sakho,Sadio Kanoute,Habib Kyombo,Clatous Chama na Kibu Denis
Akiba ni Ally,Shomary Kapombe, Joash Onyango, Victor Akpan,Okraha,Mzamiru Yassin,Dejan, John Bocco na Okwa.

Kikosi cha Yanga kwenye Ngao ya Jamii
Aziz KI ambaye ni ingizo jipya ambaye alijiunga na Yanga akitokea Klabu ya ASEC Mimosas atakutana na Okra ambaye alijiunga na Simba akitokea Klabu ya Bechem United ya Ghana.

Aidha,Yanga wanaye nyota Bernard Morrison ambaye ni mpigaji wa faulo na Simba yupo pia Nelson Okwa ambaye naye alikuwa na kazi ya kupiga mapigo huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news