Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo Agosti 13, 2022

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 13, 2022 amefanya uteuzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 13, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said imeeleza kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amefanya uteuzi huku akibadilisha uteuzi wa awali.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amebadilisha uteuzi wa Bi.Mtumwa Khatib Ameir kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Luteni Kanali mstaafu Amour Jen Ally kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said, uteuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi unaanza leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news