Maagizo ya OR-TAMISEMI yawagusa wakaguzi wa ndani

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mheshimiwa Innocent Bashungwa ameelekeza kufanywa uchambuzi wa wakaguzi wa ndani wa halmashauri ili hatua zichukuliwe kwa wasioendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassam.

"Nataka wakaguzi wa ndani wachambuliwe, wale ambao hawatoshi basi tuwachambue tuwaweke watu ambao tunaona wataendana na kasi na maelekezo ya Rais;
Bashungwa ameyasema hayo leo Agosti 2, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Ni baada ya kuibuka hoja za kujirudia miaka kadhaa katika halmashauri hizo katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini.

Katika kutekekeza hilo, amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof.Riziki Shemdoe kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango.

Pia amesisitiza inashangaza kuona kwa kipindi cha miaka minne CAG anaibua hoja zile zile katika halmashauri moja huku mkaguzi wa ndani anaendelea na kazi, licha ya kukosa ushahidi wa majibu.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Bashungwa amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kutumia mamlaka walizopewa kisheria kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wa halmashauri.

Amesema, kufanya hivyo, kutasaidia kutatuliwa kwa baadhi ya kero ndani ya halmashauri, badala ya kusubiri ziara za viongozi kutoka Serikali Kuu.

"Katibu Tawala wa Mkoa anaruhusiwa kisheria kuchukua hatua za kinidhamu kwa viongozi kabla ya kusubiri Waziri," amesema Mheshimiwa Bashungwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news