Mheshimiwa Dkt.Bärbel Kofler wa Ujerumani awasili Tanzania

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku saba kuanzia tarehe 13-20 Agosti 2022.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler (katikati) akiongozana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Dkt. Kofler alipokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga.

Katika ziara yake nchini, Dkt. Kofler pamoja na mambo mengine, anatarajia kutembelea mradi wa ajira na ujuzi kwa maendeleo ya afrika (E4D) unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani, Kituo cha malezi na mafunzo kwa wasichana wadogo ambao ni wahanga wa biashara haramu ya binadamu kilichopo Kibamba na Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akisalimiana na Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini.

Maeneo mengine atakayotembelea Naibu Waziri huyo ni pamoja na Kituo cha Afya cha Ngamiani na Hospitali ya Bombo mkoani Tanga, Zahanati ya Mkanyageni Wilayani Muheza, Halmashauri ya Jiji la Tanga, Asasi ya Tree of Hope iliyopo mkoani Tanga pamoja na Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Katika ziara yake nchini, Waziri Kofler anategemea kukutana na mawaziri wa sekta za afya, sheria, utalii, maendeleo ya jamii, fedha, nishati na maji kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news