Naibu Katibu Mkuu awapa maelekezo wataalamu Wizara ya Fedha na Mipango

NA PETER HAULE-WFM

NAIBU Katibu Mkuu Huduma za Hazina wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, amewataka wataalam wa Idara na Vitengo vya Wizara hiyo kuhakikisha wanapitia kwa umakini mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kuuboresha ili uweze kuleta tija katika utoaji huduma bora na kwa wakati kwa manufaa ya Taifa.
Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kuboresha mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara, kinachofanyika mkoani Singida.

Rai hiyo imetolewa mkoani Singida wakati akizungumza na timu ya wataalam wa wizara hiyo ambayo inapitia mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu na kuuboresha ili uweze kuwa na ufanisi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, akiwataka wataalam kutoka kwenye Idara na Vitengo vya Wizara hiyo kuwa makini wakati wa kuboresha mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara ili kuleta tija, wakati wa kikao kazi cha maboresho hayo kinachofanyika mkoani Singida.

Alisema kuwa ni vema Wizara ya Fedha na Mipango ikaonesha mfano wa kiutendaji wenye tija katika masuala ya mipango, uchumi, sera na usimamizi wa fedha na kuondoa utaratibu ambao haunatija kwa wizara, Taifa na wananchi kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Moses Dulle, akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kuboresha mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo, kinachofanyika mkoani Singida.

Alisema wizara hiyo inapofanyakazi kwa ufanisi inachochea maendeleo ya kiuchumi katika sekta nyingine na kutimiza lengo la Serikali la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news