Naibu Waziri Masanja:Serikali itakuja na mpango wa ufugaji nyuki wa Manzuki

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

SERIKALI imejipanga kuja na mpango wa ufugaji nyuki ujulikanao kama Manzuki ambapo nyuki watakuwa wanafugwa katika eneo maalum bila kuathiri uhifadhi.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb)(wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela(wa nne kutoka kulia), Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini,Mhe. Doto Biteko (wa pili kutoka kulia) pamoja na viongozi wa Serikali na chama wakiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Amefafanua kuwa kupitia mpango huo wananchi wataweza kufuga nyuki na kupata faida bila kuhama kuhama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.

Kuhusu wananchi wanaofuga nyuki katika Hifadhi ya Kigosi, amesema kuwa Serikali imeruhusu wananchi kuendelea na shughuli za ufugaji nyuki wakati inatafuta eneo mbadala la kuwahamishia wafugaji hao.

“Tamko la Serikali ni kwamba shughuli za ufugaji nyuki zitaendelea hadi pale tutakapotoa mbadala wa wapi mpeleke mizinga yenu.” Mhe. Masanja amesisitiza.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini,Mhe. Doto Biteko (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb)(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, kutoka kulia) wakati wa mkutano na wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.

Aidha, amewataka wananchi kukitumia ipasavyo Kiwanda cha kuchakata asali kilichopo katika eneo hilo ili waweze kuuza asali kwa faida.

Amewataka wananchi kutunza mazingira na kuacha kukata miti hovyo ili kuendelea kufaidika na mazao yatokanayo na nyuki.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb)(katikati) akisikiliza maelezo ya namna mitambo ya kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki inavyofanya kazi alipotembelea kiwanda hicho katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali wakifuatilia.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu masuala ya uhifadhi na ufugaji nyuki.
Awali, Waziri wa Madini na mbunge wa jimbo la Bukombe Mhe.Dkt.Doto Biteko amesema, Mhe.Rais Samia anataka kuona kero za wananchi wakiwemo wa Uyovu zinatatuliwa na ndiyo maana Mhe.Naibu Waziri amefika, hivyo kuwasihi wananchi kuwa wahifadhi kwa kuilinda misitu ya Bukombe isiharibiwe.

Naibu Waziri Mary Masanja anaendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya Maliasili na Utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news