Mufti Mkuu wa Tanzania awasihi Watanzania kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa

NA DIRAMAKINI

MUFTI Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amewasihi Watanzania wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa ambao sasa wanaendelea na zoezi la kuhesabu watu na makazi lililoanza tangu Agosti 23, 2022.
Sheikh Zubeir ametoa kauli hiyo nyumbani kwake jijini Dar es salaam, ambapo amesema yeye binafsi na familia yake tayari wameshahesabiwa ambapo ametumia nafasi hiyo kupongeza aina ya maswali yanayoulizwa na Makarani wa Sensa.

"Mimi nimeshamaliza zoezi la kuhesabiwa tena nimehesabiwa mimi na familia yangu yote na uzuri hakukua na maswali magumu yalikua maswali mepesi mepesi ambayo kila Mtanzania anayamudu kuyajibu" Amesema Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir
Aidha, Mufti Zubeir amewataka Watanzania ambao bado hawahesabiwa kwenye kuendelea kuwa watulivu kwani zoezi hilo litachukua kwa takribani siku saba hivyo Makarani watapita kwenye Kaya zao.

"Niwaambie Watanzania zoezi hili la kuhesabiwa halikua kwa siku moja tu ya Agosti 23, 2022 bali ni la siku saba kama bado hujahesabiwa basi tambua tu Karani atapita kwenye kaya na atakuhesabu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu,"ameongeza Mufti Zubeir.
Agosti 23, 2022 Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliongoza kwa mfano kushiriki zoezi la Sensa kwa kutoa taarifa sahihi kwa Karani wa Sensa aliyekwenda kumuhesabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news