NHIF yasema ipo imara, yakabidhi taarifa za wanaopotosha mitandaoni mamlaka husika

NA DIRAMAKINI

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema kumekuwepo taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii zikitoa tuhuma mbalimbali dhidi ya viongozi na watumishi wa mfuko huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 28, 2022 na NHIF ambayo imesainiwa na Kaimu Meneja Uhusiano, Bi.Grace Michael imefafanua kuwa, taarifa hizo si za kweli. "Na zina lengo ovu la kuchafua taswira nzima ya mfuko na utendaji kazi wake.

"Mfuko umechukua hatua kwa kuwasilisha taarifa kwa vyombo na mamlaka husika ili kubaini chanzo na lengo lake. Taarifa kamili itatolewa pindi suala hili litakapokamilika.

"Mfuko unawahakikishia wanachama, watoa huduma, waajiri na wadau wote wa mfuko kuwa uko imara na unaendelea na shughuli zake za kutoa huduma kama kawaida. wadau wote wa mfuko wanaombwa kuendelea kupata huduma zitolewazo na mfuko,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments