Vijana waliomaliza vyuo vikuu Musoma Vijijini waanzisha mradi wa uvuvi wa vizimba

NA FRESHA KINASA

VIJANA wanne waliomaliza masomo ya vyuo vikuu katika Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara wameamua kuanzisha uvuvi wa vizimba (aquaculture fish farming) ndani ya Ziwa Victoria eneo la Kijiji cha Bujaga Kata ya Bulinga.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 28, 2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ikielezea hatua hiyo njema kwa vijana hao.

Hatua hiyo, inalenga kuwafanya kuwa na kipato ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi na kumudu kuendesha maisha yao kwa kujiajiri ili kujipatia kipato.

Kiongozi wa kikundi hicho, Albert Simon ana Shahada ya Elimu ambapo amemuomba Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo aweze kuwasaidia kupata msaada au mkopo wa serikali.

Ambapo mkopo huo utawawezesha kupanua mradi wao wa uvuvi wa vizimba ambao ndio ajira yao ili pia waweze kuajiri vijana wengine wa Kata ya Bulinga Halmashauri ya Musoma Vijijini.
Aidha,ombi lao tayari limefikishwa serikalini na kwamba mradi huo utaongozwa na kijana, Simon Albert katika Kijiji cha Bujaga Kata ya Bulinga.

Post a Comment

0 Comments