Parimatch yaidhamini tena Mbeya City FC

NA DIRAMAKINI

KAMPUNI ya kubasishiri ya Parimatch na uongozi wa klabu ya Mbeya City imesaini mkataba wa udhamini kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Afisa Habari wa Parimatch, Ismail Mohamed amesema kuwa, kampuni ya inayoendesha shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni, leo imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Amesema kuwa, hii ni mara ya pili kwa kampuni yao kudhamini Mbeya City, hususani ukiangalia idadi ya mashabiki na ushawishi na ndiyo kurejea kwao kufanya udhamini. na kutoa vifaa vya michezo na kufanya ukarabati uwanja wa Sokoine.

Amesema kuwa, Kampuni ya Parimatch moja ya jukumu lao michezo inakuwa kuanzia ngazi ya chini mpaka Kimataifa.

Mohamed amesema, wameamua kuunga mkono Mbeya City, ili wapenzi wa soka waendelee kupata burudani stahiki.

Mohamed Ismail amesema katika udhamini huo wa msimu mmoja Parimatch inatoa pesa taslim, vifaa kwa ajili ya klabu pamoja na ukarabati wa Uwanja wa Sokoine, hasa katika eneo la kukaa benchi la ufundi.

"Parimatch licha ya kuidhamini Mbeya City, ambayo inashiriki Ligi ya Kuu YA nbc Tanzania Bara, pia tunaidhamini Chelsea na Leicester City ambazo zinashiriki Ligi ya Uingereza,"amesema Mohamed.

Afisa huyo wa Habari alisema kuwa anawashukuru wadau was soka. nchini ikiwa ni pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Michezo na Mbeya City kwa kuwapokea kama wadau rasmi wa michezo.

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema, kwa upande wao wamefurahishwa na udhamini huo ambao utazidi kuipa chachu ya kufanya vizuri zaidi kwenye msimu mpya unaotarajia kuanza Agosti 15.

Amesema, Parimatch waliwadhamini msimu wa 2020/21 hivyo kurudi kwao msimu huu, kumetokana na kuridhishwa kwao na udhamini huo uliopita.

"Tunashukuru kwa kupata udhamini huu, maana bado wanaendelea kutumiani, tulikuwa nao wameridhika na kutupa tena nafasi nyingine, tuna imani kubwa ya kufanya vizuri kupitia udhamini huu,"amesema Kimbe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news