Rais Samia afanya uteuzi, ampa Prof.Mwandosya jukumu EWURA

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua Prof.Mark James Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 19, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo unaanza Agosti 15, 2022 huku Prof. Mwandosya akichukua nafasi ya Prof,Jamidu Hazzam Yahaya ambaye amemaliza muda wake.


Post a Comment

0 Comments