Rais Samia afanya uteuzi MSCL, TBC

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua, Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).
Kabla ya uteuzi huo, Hamissi alikuwa nje ya uteuzi baada ya kutenguliwa katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Julai 4, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo unaanza Agosti 4, 2022.

Mbali na Hamisi mwingine aliyeteuliwa ni Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

"Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert Mrango ambaye amemaliza kipindi chake," imeeleza taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Kagaigai alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, kabla ya kuachwa Julai 28, 2022, katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa. Aidha, Kagaigai amewahi kuwa Katibu wa Bunge la Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news