Rais Samia atoa maagizo kwa halmashauri yanayolenga kudhibiti migogoro ya wakulima, wafugaji

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziagiza halmashauri za Mkoa wa Iringa kutambua maeneo ya malisho na kuyapima ili kupunguza muingiliano wa matumizi ya ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji.

Rais Samia ametoa agizo hilo Agosti 12, 2022 wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Samora.

Aidha, Rais Samia amewataka wananchi wafuge kwa kufuata kanuni za ufugaji bora na kuendelea kuelimishwa kufuga kibiashara kwa kuzingatia mahitaji ya soko ili kupata manufaa makubwa.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali inatambua mchango wa Mkoa wa Iringa katika kilimo kwa nchi, hivyo inachukua hatua anuwai kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo kwa gharama nafuu.

Vile vile, Rais Samia amesema Serikali imeweka ruzuku kwenye mbolea za kupandia na kukuzia ili kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima.

Serikali imeongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 294 mwaka 2021/22 hadi kufikia shilingi bilioni 954 mwaka 2022/23 ili wakulima wazalishe mazao ya kilimo kwa tija na wananchi wote wanufaike na kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news