NA DIRAMAKINI
WANAWAKE wajane wameendelea kuunganisha nguvu ya pamoja kupitia chama chao, Chama cha Wanawake Wajane Tanzania (CCWWT) kuanzia ngazi za chini hadi Taifa.

Hayo yamebainika Agosti 12, 2022 baada ya Mwenyekiti wa CCWWT Taifa,Bi.Rabia Ally Moyo kushiriki katika uzinduzi wa chama hicho tawi la Tandale kwa Tumbo lililopo Kata ya Tandale ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inawathamini ndiyo maana aliunda wizara ambayo pamoja na mambo mengine, kundi la wajane limetajwa kama sehemu ya kusimamiwa na wizara hiyo.