Simba SC yaichapa Asante Kotoko mabao 4-2

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha Simba SC kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana.

Ni mchezo uliopigwa Agosti 28, 2022 katika dimba la Al Hilal nchini Sudan ambapo katika mchezo huo Steven Mukwala aliwapatia Kotoko bao la kwanza dakika ya tisa baada ya walinzi wa Simba SC kuchelewa kuondoa hatari.

Augustine Okrah aliwasawazishia Simba SC bao hilo dakika ya 19 baada ya kumalizia pasi ya mlinzi wa kulia Israel Patrick.

Pape Sakho alitupatia bao la pili dakika ya 26 baada ya kuwapiga chenga walinzi wa Asante Kotoko na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango.

Naye Clatous Chama alitupia la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya Moses Phiri kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Chama alitupatia bao la nne dakika ya 55 baada ya kumpiga chenga mlinzi mmoja wa Asante Kotoko kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Peter Banda.

Steven Amankona aliwapatia Kotoko bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 78 baada ya Nassor Kapama kufanya madhambi ndani ya 18.

Katika mtanange huo, Kocha Zoran Maki aliwatoa Mohamed Ouatara, Phiri, Chama, Sakho na Ally Salim na kiwaingiza Peter Banda, Dejan Georgijevic, Jimmyson Mwanuke, Nelson Okwa na Ahmed Feruz.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news