TANESCO kuzima mfumo wa kununua LUKU kwa siku nne, hakuna atakayeweza kununua umeme

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la UmemeTanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wa malipo ya kabla (LUKU).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 17, 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano na Masuala ya Umma TANESCO makao makuu jijini Dodoma.

"Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 4 kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 22 hadi 25 Agosti 2022, muda wa saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi. Katika muda wa zoezi hili wateja hawataweza kununua umeme kupitia mfumo wa LUKU.

"Shirika linawashauri wateja wake kununua umeme wa ziada, au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.

"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza,"imefafanua taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news