Vijana saba wafungua zahanati kupitia mkopo wa halmashauri

NA MWANDISHI WETU

VIJANA saba ambao ni wataalam wa afya pamoja na mwanasheria mmoja kutoka katika Jiji la Dar es Salaam wamejiajiri kwa kufungua zahanati kupitia mkopo wa halmashauri.
Zahanati hiyo wameifungua Kipunguni kwa Mkolemba Halmashauri ya Wilaya ya Ilala baada ya kupatiwa shilingi milioni 110 ambazo ni sehemu ya mkopo utokanao na ukusanyaji wa mapato ya asilimia 10 ya halmashauri.
Miongoni mwa vijana hao kati yao wamo madaktari wawili, mfamasia mmoja, wataalam wa maabara wawili, manesi wawili na mwanasheria mmoja ambapo jana zahanati yao imezinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Jerry Silaa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Silaa amesema, "nimepewa ulezi, nitawalea kwa moyo na kuhakikisha wamekuwa.Huu ni mfano halisi wa kazi kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwatengenezea vijana mazingira ya kujiajiri. Mikopo ya halmashauri inalipa jiongeze na kuwa mbunifu,"amesema.

Post a Comment

0 Comments