Rais Samia afanya uteuzi UDSM, NECTA

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi kama ifuatavyo:

Mosi, amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Mhe. Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.

Pili,amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Prof. Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.

Hayo ni kwa mujibu wa taraifa iliyotolewa leo Agosti 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo ameeleza kuwa, uteuzi huo unaanza Agosti 23, 2022.

Post a Comment

0 Comments