NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) ikinunuliwa kwa shilingi 624.31 na kuuzwa kwa shilingi 630.52.

Hayo ni kwa mujibu wa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Agosti 5, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 136.94 na kuuzwa kwa shilingi 138.27 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.26 na kuuzwa kwa shilingi 19.42.

Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2332.94 na kuuzwa kwa shilingi 2357.20 huku Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2293.04 na kuuzwa kwa shilingi 2315.98.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 339.42 na kuuzwa kwa shilingi 342.73 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.15 na kuuzwa kwa shilingi 17.32.
0 Comments