Wanasheria wamefanya imewezekana na wanahabari inawezekana pia-Waziri Nape

NA MWANDISHI WETU

“Tulipotunga Sheria ya mwaka 2016, lengo lake ilikuwa ni kwamba tupunguze mikono ya Serikali kuendesha vyombo vya habari Serikali iliamini kwamba ikipita njia hiyo, itakuwa imefanikiwa kupunguza madaraka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo aliyopewa na sheria ya mwaka 1976.

“Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), ndiye mwakilishi wa Serikali katika kusimamia vyombo vya habari, tunataka madaraka yake yapungue kadri inavyowezekana;

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye ameyasema hayo Agosti 24, 2022 katika mahojiano katika kipindi cha Dira ya Dunia cha runinga ya BBC.

Amesema kuwa, sehemu kubwa ya usimamizi wa vyombo vya habari ibaki kwa wanataaluma wenyewe tofauti na sheria ya habari ya mwaka 1976 ambayo iliingiza mikono mingi katika kusimamia vyombo vya habari.
“Sheria hii tukatamani ipunguze, na namna ya kupunguza ilikuwa ni pamoja na kuunda Baraza Huru la Wanahabari ili yale ya kitaaluma wayamalize huko,"amesema.

Mheshimiwa Waziri Nape amesema kuwa, waandishi wa habari kama wanataaluma wengine wakiwemo wanasheria wajisimamie wenyewe, na kwa hilo inawezekana.

“Sisi kama serikali tubaki na vitu vichache sana vinavyolinda nchi, usalama na afya ya jamii.Lakini mengine mengi yafanywe na wanahabari wenyewe na inawezekana maana madaktari wamefanya imewezekana, wanasheria wamefanya imewezekana na wanahabari inawezekana,”amesema Mheshimiwa Waziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news