Watakiwa kusimamia rasilimali watu ili kuinua pato la Taifa kupitia filamu ya The Royal Tour

NA VERONICA E.MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama amewaelekeza Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanasimamia vema utendaji kazi wa watumishi wa umma ili kuongeza pato la taifa kupitia filamu ya ‘The Royal Tour’ iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Laban Thomas wakati wa tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo wakati wa akizindia rasmi tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour” katika Mkoa wa Ruvuma iliyoasisiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi.

Waziri Jenista amesema, viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, uzalendo na uadilifu katika kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii, na kuongeza kuwa viongozi Serikalini hawana budi kusimamia kikamilifu utendaji kazi ili kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

“Niwaombe viongozi wenzangu kila mmoja wetu katika eneo lake la kazi, asimame na ajenda ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais za kuchangia maendeleo ya taifa kwa kufanya kazi kwa bidii, uzalendo na uadilifu.” Mhe. Jenista amesisitiza.

Katika suala la ukusanyaji mapato mkoani Ruvuma, Mhe. Jenista amewakumbusha viongozi hao kupanua wigo wa ukusanyaji mapato kwa kutumia mifumo madhubuti ya TEHAMA ya ukusanyaji mapato, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kulipa kodi kwa hiari ili kuongeza pato la Taifa.
Baadhi ya Watumishi wa Umma mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Aidha, Mhe. Jenista amewasisitiza viongozi hao kusimamia kikamilifu mfumo mpya wa ruzuku ya mbolea ulioasisiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili uwafikie wananchi kwa utaratibu uliopangwa na Serikali na uwe na manufaa kwenye kilimo.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa katika eneo hili, hatutegemei kusikia kazi hii nzuri iliyofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya mfumo wa ruzuku ya mbolea umeingiliwa na rushwa, tusimame imara ili mfumo huu umfikie kila mlengwa kwa utaratibu uliopangwa na Serikali.” Mhe. Jenista amesisitiza.

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kwenye tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Laban Thomas akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na viongozi na wananchi wakati wa tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kwenye tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ katika uwanja wa Majimaji Mkoa wa Ruvuma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya Nyara za Serikali kutoka kwa Afisa Utalii Pori la Akiba Liparamba, Bi. Maajabu Mbogo wakati wa tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akicheza ngoma ya Mganda kwenye tamasha la kuenzi mchango wa filamu ya ‘The Royal Tour’ lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na viongozi na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Laban Thomas amesema kufanyika kwa tamasha hilo mkoani Ruvuma ni sehemu ya kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais kwa maono yake makubwa ya kuamua kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya ‘The Royal Tour’ ili kuwavutia watalii na wawekezaji mbalimbali kutoka pande zote za dunia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua filamu ya ‘The Royal Tour’ tarehe 28 Aprili, 2022 jijini Arusha yenye lengo la kuvutia watalii na uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news